KWA:   WATANZANIA WOTE WAISHIO KUWAIT

 

Ubalozi unapenda kuwafahamisha/kuwajulisha kuwa mabadiliko ya bei itakayotozwa katika huduma ya hati ya dharura ya kusafiria (Emergency Travel Document) imepanda na kuwa dola za Kimarekani Ishirini (USD 20) badala ya dola za Kimarekani kumi (USD 10) iliyokuwa ikitozwa awali.

Aidha, huduma ya kupata pasipoti mtandao (electronic passport) itatolewa Balozini, mtajulishwa taratibu zote pindi Ubalozi utakapoanza kutoa huduma hiyo.

Ukipata taarifa hii, mjulishe na mwenzio!

 

Tunawashukuru kwa ushirikiano wenu!

 

BY: UTAWALA

19/5/2019